9 Jun 2016

Taarifa ya Muhula wa Kwanza-2016

Salamu kutoka Mang'ola,

Tumefikia mwisho wa muhula wa Kwanza (kwa O-level) na muhula wa Pili (kwa A-level) mwaka 2016.

Wanafunzi wote wamefanya mitihani yao na karatasi kusahihishwa na wamerudishiwa.

Shule itafungwa Ijumaa, tarehe 10 Juni 2016, na wanafunzi wote watondoka shuleni.

Shule itafunguliwa Jumamosi, tarehe 16-7-2016 kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Mang'ola na Jumapili, tarehe 17-7-2016 kwa wanafunzi wanaotoka Mang'ola. Wanafunzi wawahi kufika. Wale wanaotoka nje ya Mang'ola wafike kabla ya saa 11 jioni na wale wanaotoka Mang'ola wafike kabla ya saa tisa alasiri. Wanafunzi watakaochelewa watarudishwa nyumban siku hiyo hiyo.

Ni muhimu wanafunzi wafike wakiwa wamelipa ADA, watakaolipa benki wafike na "pay-slip." Pay slip iandikwe JINA KAMILI na KIDATO cha mwanafunzi anayelipiwa. Fedha ya MICHANGO, NAULI, MITIHANI, n.k. ilipwe taslimu.

MUHIMU:

  1. Ada ya A-level (kidato cha 5 & 6) imeongezeka kutoka sh. 600,000/- mwaka jana hadi sh. 700,000/- mwaka 2016/2017.
  2. Michango (administrative contributions) imeongezeka sh. 22,000/- kutokana na agizo la Jimbo kuchangia sh 30,000/- kwa kila mwanafunzi kwa ajili ya uendeshaji wa idara ya Elimu.
----
Utawala

How to reach Us

Mang'ola Chini
-----------------------
P. O. Box 389
KARATU - ARUSHA
TANZANIA
-----------------------
Tel : +255 (0) 27 253 4129
Mob : +255 783 4444 89
-----------------------
Email : annagamazo(dot)school(at)gmail(dot)com
-----------------------
All Correspondence should be addressed to the "Headmistress"