20 Jul 2015

Shule yetu ni "Number 1!"

Shule yetu ni ya KWANZA katika matokeo ya Mtihani wa ACSEE (Kidato cha Sita) mwaka 2015!

Kama majedwali hapo juu yanavyoonesha, Anna Gamazo Sekondari ni ya KWANZA katika mkoa wa Arusha kwa shule zenye wanafunzi chini ya 30 na ni namba 21 kitaifa! Pia somo la Jiografia (Geography) limeshika nafasi ya Kwanza kimkoa na ya 12 kitaifa bila kusahau somo la Kiswahili lililoshika nafasi ya Pili kimkoa. Tunawapongeza wahitimu wetu, wazazi na walezi wao, walimu na uongozi mzima wa Shule kwa kuweza kufanikiwa kufikia mafanikio haya makubwa.

Shule inaendelea kuwaahidi juhudi zaidi katika uboreshaji wa mazingira ya kujifunza na kufundishia kwa kuimarisha miundombinu, nidhamu, mbinu na vifaa vya ufundishaji na motisha ili kuiendeleza shule na kuweza kupata mafanikio ya kiwango hiki na bora zaidi kila wakati na kwa kila jambo!

KARIBU ANNA GAMAZO SEC.!

How to reach Us

Mang'ola Chini
-----------------------
P. O. Box 389
KARATU - ARUSHA
TANZANIA
-----------------------
Tel : +255 (0) 27 253 4129
Mob : +255 783 4444 89
-----------------------
Email : annagamazo(dot)school(at)gmail(dot)com
-----------------------
All Correspondence should be addressed to the "Headmistress"