5 Jun 2015

Maadhimisho ya World Environment Day - 2015

Salamu kutoka Mang'ola,


Tarehe 5 ya mwezi Juni kila mwaka ni Siku ya Umoja wa Mataifa ya Mazingira duniani. Hapa shuleni siku hiyo iliadhimishwa kwa uratibu wa Klabu ya MaliHai. Ambapo katika ukumbi wa Shule (Auditorium), kulikuwa na nyimbo, mashairi na ngonjera juu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira.
Mwalimu mlezi wa Klabu ya MaliHai, Bw Mwambenja



Wana-ASA tawi la hapa shuleni wakiwakilisha wimbo maalumu kabisa wa kutukuza uumbaji wa Mungu.

Sehemu ya wanafunzi wakifuatilia hotuba.

F2 wakiimba shairi.

Mgeni rasmi, mwanamazingira na mdau wa utalii Bw. Christian Schmeling wa Kisimangeda Camp

(L-R) Sr Mercy, Mr. Sangida, Mr. Christian, Ms Hosiana na Pd Miguel wakishuhudia upandaji wa mti.
Pia kulikuwa na hotuba mbalimbali kutoka kwa wageni waalikwa akiwemo Pd Miguel ambaye pia ni meneja wa Shule na mgeni rasmi, mdau wa Mazingira na Utalii Bw. Christian Schmeling wa Kisimangeda Camp.


Kaulimbiu ya WED 2015 ya "Seven Billion Dreams. One Planet. Consume with Care" ilisisitizwa kwenye salamu za mwalimu Mlezi wa Klabu Bw. Mwambenja. Pia alisisitiza umuhimu wa kutumia na kutunza rasilimali kwa kufuata kanuni za uhifadhi na uendelevu.

Meneja wa Shule akipanda mti wa kumbukumbu.

Mwenyekiti wa Klabu ya MaliHai akipanda mti wa kumbukumbu.

How to reach Us

Mang'ola Chini
-----------------------
P. O. Box 389
KARATU - ARUSHA
TANZANIA
-----------------------
Tel : +255 (0) 27 253 4129
Mob : +255 783 4444 89
-----------------------
Email : annagamazo(dot)school(at)gmail(dot)com
-----------------------
All Correspondence should be addressed to the "Headmistress"