26 Oct 2020

13 Jul 2018

11 Jan 2018

24 Jan 2017

4 Jan 2017

Taarifa ya Muhula wa Kwanza 2017

Salamu kutoka Anna Gamazo Sekondari. 

Heri na fanaka za Mwaka Mpya 2017.

Shule itafunguliwa Ijumaa, tarehe 6 kwa wanafunzi wanaotoka Mang'ola na Jumamosi, tarehe 7 kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Mang'ola. Wanafunzi wawahi kufika shuleni, wataochelewa watarudishwa nyumbani siku hiyo hiyo bila kujali wametoka wapi.

Mzazi/mlezi hakikisha kuwa:

  1. Mwanao anafika amelipa karo na michango (ikiwa imelipwa benki na afike na pay-in slip ya benki ikiwa na majina yake na kidato)
  2. Mwanao anafika akiwa na ripoti yake ikiwa imesainiwa na kuwekwa maoni yako mzazi/mlezi. Ili kubakiwa na kumbukumbu unaweza kutoa nakala (photocopy).
  3. Mwanao anafika shuleni kwa wakati bila kuchelewa ili kuepusha kurudishwa nyumbani.
  4. Mwanao hafiki na vitu visivyoruhusiwa kama vile losheni, laini za simu, glycerine, poda na nguo zisizopaswa. Mkague mwanao kabla hajaondoka nyumbani. Pia awe amenyoa kufuatana na maagizo ya Shule ambayo mwanao anayafahamu (MUHIMU SANA Asichonge kichwa)
Kutakuwa na ENTRY TESTS  kuanza Jumatatu, tarehe 9 hivyo hakikisha mwanao hachelewi kufika shuleni.

15 Jul 2016

Matokeo ya Kidato cha Sita - 2016

Salamu kutoka Mang'ola

  1. Muhula wa pili (na wa kwanza kwa A-level) utaanza tarehe 18 Julai 2016. Kutakuwa na mitihani (entry exams) wiki hiyo, hivyo wanafunzi wasichelewe kurudi shuleni.
  2. NECTA wametoa matokeo ya Kidato cha Sita - 2016. Shule yetu imeendelea kufanya vizuri kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.

9 Jun 2016

Taarifa ya Muhula wa Kwanza-2016

Salamu kutoka Mang'ola,

Tumefikia mwisho wa muhula wa Kwanza (kwa O-level) na muhula wa Pili (kwa A-level) mwaka 2016.

Wanafunzi wote wamefanya mitihani yao na karatasi kusahihishwa na wamerudishiwa.

Shule itafungwa Ijumaa, tarehe 10 Juni 2016, na wanafunzi wote watondoka shuleni.

Shule itafunguliwa Jumamosi, tarehe 16-7-2016 kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Mang'ola na Jumapili, tarehe 17-7-2016 kwa wanafunzi wanaotoka Mang'ola. Wanafunzi wawahi kufika. Wale wanaotoka nje ya Mang'ola wafike kabla ya saa 11 jioni na wale wanaotoka Mang'ola wafike kabla ya saa tisa alasiri. Wanafunzi watakaochelewa watarudishwa nyumban siku hiyo hiyo.

Ni muhimu wanafunzi wafike wakiwa wamelipa ADA, watakaolipa benki wafike na "pay-slip." Pay slip iandikwe JINA KAMILI na KIDATO cha mwanafunzi anayelipiwa. Fedha ya MICHANGO, NAULI, MITIHANI, n.k. ilipwe taslimu.

MUHIMU:

  1. Ada ya A-level (kidato cha 5 & 6) imeongezeka kutoka sh. 600,000/- mwaka jana hadi sh. 700,000/- mwaka 2016/2017.
  2. Michango (administrative contributions) imeongezeka sh. 22,000/- kutokana na agizo la Jimbo kuchangia sh 30,000/- kwa kila mwanafunzi kwa ajili ya uendeshaji wa idara ya Elimu.
----
Utawala

How to reach Us

Mang'ola Chini
-----------------------
P. O. Box 389
KARATU - ARUSHA
TANZANIA
-----------------------
Tel : +255 (0) 27 253 4129
Mob : +255 783 4444 89
-----------------------
Email : annagamazo(dot)school(at)gmail(dot)com
-----------------------
All Correspondence should be addressed to the "Headmistress"