4 Jan 2017

Taarifa ya Muhula wa Kwanza 2017

Salamu kutoka Anna Gamazo Sekondari. 

Heri na fanaka za Mwaka Mpya 2017.

Shule itafunguliwa Ijumaa, tarehe 6 kwa wanafunzi wanaotoka Mang'ola na Jumamosi, tarehe 7 kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Mang'ola. Wanafunzi wawahi kufika shuleni, wataochelewa watarudishwa nyumbani siku hiyo hiyo bila kujali wametoka wapi.

Mzazi/mlezi hakikisha kuwa:

  1. Mwanao anafika amelipa karo na michango (ikiwa imelipwa benki na afike na pay-in slip ya benki ikiwa na majina yake na kidato)
  2. Mwanao anafika akiwa na ripoti yake ikiwa imesainiwa na kuwekwa maoni yako mzazi/mlezi. Ili kubakiwa na kumbukumbu unaweza kutoa nakala (photocopy).
  3. Mwanao anafika shuleni kwa wakati bila kuchelewa ili kuepusha kurudishwa nyumbani.
  4. Mwanao hafiki na vitu visivyoruhusiwa kama vile losheni, laini za simu, glycerine, poda na nguo zisizopaswa. Mkague mwanao kabla hajaondoka nyumbani. Pia awe amenyoa kufuatana na maagizo ya Shule ambayo mwanao anayafahamu (MUHIMU SANA Asichonge kichwa)
Kutakuwa na ENTRY TESTS  kuanza Jumatatu, tarehe 9 hivyo hakikisha mwanao hachelewi kufika shuleni.

How to reach Us

Mang'ola Chini
-----------------------
P. O. Box 389
KARATU - ARUSHA
TANZANIA
-----------------------
Tel : +255 (0) 27 253 4129
Mob : +255 783 4444 89
-----------------------
Email : annagamazo(dot)school(at)gmail(dot)com
-----------------------
All Correspondence should be addressed to the "Headmistress"