29 Oct 2014

Nyerere day 2014

The main event of the day was panel discussion session on "15 years after Nyerere's death. Are we honouring his legacies?"

Wanafunzi wakiwa wanasikiliza kwa makini "Panel discussion" iliyoandaliwa na English Dept na kuongozwa na wanafunzi.

Mmoja wa washindi wa mashindano ya kuutunga ushairi (Poems) akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Shule, Sr. Mercy Stella na mkuu wa Idara ya somo la Kiingereza, Mwl. V Labia.

Washindi wa uandishi wa Insha na Ushairi wakiwa na vyeti vyao vya ushindi. (Vyeti vya njano, ushairi na vyeti vya rangi ya chungwa, insha.)
Siku ya Nyerere (Nyerere day) mwaka 2014 iliandaliwa na Idara ya somo la Kiingereza (English Dept) ambapo ilihusisha uandishi wa Insha na Ushairi (Essay writing and poem composition). 

Wanafunzi wote walialikwa kuandika insha kuhusu moja kati ya mada zifuatazo:
  1. The re-introduction of compulsory National Service (JKT)
  2. Tanzania towards getting a new Constitution
Pia kutunga ushairi kuhusu "The legacy and life of Mwl. JK Nyerere". Jumla ya insha 70 ziliwasilishwa kwa majaji kwa ajili ya mashindano na zaidi ya mashairi 200 pia yaliwasilishwa. 

Tukio kubwa la siku lilikuwa ni panel discussion, iliyoongozwa na kuendeshwa na wanafunzi 14 waliowakilisha vidato vyote.  Yalikuwa majadiliano marefu, yenye ari na mwamko na yenye kuonesha uelewa wa wanafunzi wetu kumhusu Baba wa Taifa na hatima yao kama vijana katika taifa hili.

Baadae wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa ushairi waliyasoma mashairi yao yaliyoshinda mbele ya hadhira na kutunukiwa vyeti na mkuu wa Shule, wanafunzi waliofanya vizuri kwa upande wa Insha pia walitunikiwa vyeti.

Idara ya somo la Kiingereza ambao ndio waandaaji wa tukio hili inajivunia mafanikio yake na inatarajia kulifanya tukio hili kuwa la kudumu kwenye kalenda ya matukio ya Idara na kuboresha zaidi maandalizi yake, kwani wanafunzi wameweza kupata wasaa na fursa ya kuboresha matumizi ya lugha ya Kiingereza kwa kuandika, kutunga na kuzungumza.

Mwl. V. Labia (HoD - English Dept)

How to reach Us

Mang'ola Chini
-----------------------
P. O. Box 389
KARATU - ARUSHA
TANZANIA
-----------------------
Tel : +255 (0) 27 253 4129
Mob : +255 783 4444 89
-----------------------
Email : annagamazo(dot)school(at)gmail(dot)com
-----------------------
All Correspondence should be addressed to the "Headmistress"