13 Jan 2015

Salamu za Mwaka Mpya 2015

Heri ya Mwaka Mpya 2015 kutoka kwa Bodi ya Shule, uongozi wa Shule, walimu na wafanyakazi wasiokuwa walimu na wanafunzi wote!

  • Mwaka wa masomo umeanza tarehe 13 Januari, wanafunzi wamekwishafika na wameanza "Entry tests" zitakazo endelea hadi Ijumaa, tarehe 16.
  • Mradi mkubwa uliohusisha kufunga pampu ya umeme kuleta maji kutoka mtoni, umekamilika na unafanya kazi kwa 100%. Hivyo wanafunzi watapata maji kwa matumizi yao hapa hapa shuleni, bila kuhitaji kwenda mtoni. Tunamshukuru Mungu, wafadhali na meneja wa Shule kwa kuweza kufanikisha mradi huu!
  • Kazi ya kuleta umeme wa gridi (TANESCO) inaendelea na kuligana na maelezo ya mkandarasi wa mradi huo, umeme utakuwa umefika hadi kufikia mwisho wa mwezi wa pili. Tunaamini kukamilika kwa mradi huo wa umeme utaendelea kusaidia taasisi katika kufanikisha kuweza kutoa huduma iliyo bora zaidi.
  • Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Maandalizi (Orientation course) wanapaswa kuripoti bila kukosa tarehe 7 mwezi Februari 2015, saa tatu asubuhi. Tafadhali fika na yafuatayo:
  1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa (birth certificate) au cheti cha ubatizo kwa ajili ya uhakiki wa taarifa za mwanafunzi
  2. Stakabadhi ya benki (bank pay-in slip) ya malipo ya ada (KUMBUKA: Karo pekee ndiyo ilipwe kupitia benki na sio michango mingine)
  3. Mahitaji yote muhimu kama yalivyo oneshwa kwenye fomu ya maagizo ya kujiunga na shule.
KUTAKUWA NA KIKAO KIFUPI CHA WAZAZI, HIVYO NI MUHIMU SANA KUFIKA MZAZI/MLEZI WA MTOTO BILA KUKOSA AU KUCHELEWA
  • Wanafunzi waliochaguliwa (au waliopata nafasi ya kuhamia kidato cha Kwanza na cha Tatu (Form I & III), wanapaswa kufika shuleni tarehe 14 na 15 Januari. Tafadhali wafike wakiwa na mahitaji yote muhimu kama yalivyooneshwa kwenye maagizo ya kujiunga.
Baada ya taarifa hizo, kwa niaba ya wafanyakazi na uongozi wote wa Shule, nawatakia fanaka na baraka za mwaka 2015 na ninatarajia kama wadau wa shule hii mtaendelea kuonesha ushirikiano kwangu na kwa taasisi kama mlivyofanya mwaka uliopita.
 
- Sr. Mercy Stella (SAS)

How to reach Us

Mang'ola Chini
-----------------------
P. O. Box 389
KARATU - ARUSHA
TANZANIA
-----------------------
Tel : +255 (0) 27 253 4129
Mob : +255 783 4444 89
-----------------------
Email : annagamazo(dot)school(at)gmail(dot)com
-----------------------
All Correspondence should be addressed to the "Headmistress"